| Vuta nikuvute ya wamiliki wa bendi juu ya mwanamuziki Kalala Junior aliyekuwa bendi ya Mapacha Watatu yazidi kushika kasi. Kiongozi wa bendi ya Mapacha Watatu , Jose Mara amesema kwamba bendi hiyo, ingawa ameondoka mmoja kati yao lakini hatobadili jina kuitwa mapacha wawili, au kuchukuwa msanii yoyote mkubwa kwaaajili ya kuziba pengo hilo. Jose Mara amesema bendi hiyo jina la Mapacha Watatu lipo kama jina la usajili, na wala halibadiliki hata kama wakiondoka wote, hata hivyo amesema kuondoka kwa mwenzao mmoja wao bado wanaendelea kusonga, na hivi karibuni wametoa wimbo Ona Naonewa wakimshirikisha Ali Kiba. Pia walisisitiza na kusema hivi sasa watakuwa wakichukuwa wasanii wachanga na kuwakuza wenyewe ambapo kwa sasa wanaye Jemsi Mavoko, Kambi Catherine, Adam wa Tabata na wengine wengi ambao wanafanya vizuri. Hata hivyo mwuisho walimalizia kwa kusema hawajui mwanamuziki huyo wapi anaelekea. |
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi