Wednesday, August 15, 2012

Super Nyamwela atunukiwa cheti cha ualimu wa kimataifa

Bendi ta Extra Bongo ambayo mnenguaji wake mashuhuri hapa jijini Dar es salaam na Tanzania kwa ujumla Super Nyamwela, juzi walikuwa Finland katika tamasha maalum ambalo ambayo waliweza kufana show katika miji mbalimbali. Hata hivyo mnenguaji huyo, aliweza kuchaguliwa na wazungu kufundisha katika chuo kikuu cha nchi hiyo kinachoitwa Helensink University, ambapo kipo katika mji huo na chuo kingine kilichopo katika mji wa Tempere. Nyamwela anasema zilimchukuwa wiki mbili kufundisha wazungu, ambao wapo waliokuja kujifunza kwa lengo la mazoezi na wapo waliokuja kujifunza kwa lengo la kazi. anasema kutokana na mazoezi hayo, wakampa nafasi kwamba watakuwa wanamchukuwa nchini humo kwaajili ya kuwafundisha, kwahiyo kuanzia sasa Super Nyamwela muda na saa yoyote anaweza kuchukuliwa kwenda Finland kwaajili ya kufundisha Africana Dance
 Wakati huo kiongozi wa Bendi ya Extra Bongo, Ali Choki 'Mzee wa Scandnavia' anasema katika sikuu ya Idd wanatarajia kuizindua alamu yao itakayokuwa na nyimbo saba, lakini hakusema albamu hiyo itakuwa na jina gani.
 Mwanamuziki Banza Stone, naye alisema mambo yake yote anasubiri pindi uzinduzi ukifanyika ndipo aonyeshe kazi zingine atakazo kuja nazo.





Wanamuziki wa Extra Bongo

No comments:

Post a Comment

https://www.facebook.com/gomesamohamedi