Mwigizaji wa filamu za kuchekesha nchini Athuman 'Amri Kingi Majuto' amesema kwa sasa yupo Mwanza kwaajili ya kutoa elimu juu watu wenye ugonjwa wa ngozi jinsi wanavyokuwa na kwanini inatokea hivyo. Majuto alisema mradi huo mara kwanza alikuwa akiufanya Mzee Small pamoja na Bi Chau, lakini aliuchukuwa yeye pamoja na Bi Chau, baada ya mzee huyo kuugua presha ambayo imemsabishia ugonjwa wa kiarusi. Majuto amesema tarehe 20 mwezi huu mradi huo utakuwa unafikia mwisho na yeye kurudi tena kwenye kazi yake ya kuchekesha kama ilivyokuwa zamani. Ameongeza kwa kusema mradi huo tayari wameshatembelea mikoa mbalimbali kwajili ya kutoa elimu, pamoja na dawa kwa wagonjwa wa ngozi ambao wanajulikana kama Albino.

No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi