| Mwigizaji Jack ambaye aliigiza kama Jini katika filamu ya Penzi la Kiza, akiwa katika moja ya uigizaji wake katika filamu hiyo. Uchukuaji wa picha wa filamu hiyo tayari umeshakamilika, na hivi sasa ipo katika mikakati ya kuweka picha vizuri na kuzifanyia mautundu kwaajili ya kuingia sokoni. Ni filamu ambayo inaelezea zaidi masuala ya uchawi, kisa cha mapenzi na matukio ya ajabu ambayo unaweza mtu kufanyiwa bila ya kujua kama unafanyiwa. Pia inaonyesha kwamba uadui si lazima mtu awe adui yako ndiyo akufanyie uadui, hata yule unayemwamini anaweza kuwa adui. Si ya kuikosa, subiri yaja |
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi