| Unaposikia King, basi watu wanamaanisha King na huyo aliyempa jina hili hakukosea hata kidogo. Wanamwita King Majuto, safari hii akiwa na Jacob Stephan 'JB' ndani ya filamu ya NAKWENDA KWA MWANANGU. Kama lilivyolengo la Jb kwamba filamu zake za sasa zote zitakuwa katika mtindo wa Seriasi komedi, yaani nusu kichekesho nusu umakini, ndivyo alivyofanya filamu hii. Kwa upande unaweza kusema hawa watu waposiriasi kwa jambo wanalolifanya, lakini vituko vya wao wenyewe vitakufanya kuona hili ni bonge la kichekesho. King Majuto siku zote amezooleka kwa filamu za kuchekesha, lakini sasa amezidikuchekesha huenda zaidi ya mwanzo. Kweli mwache aitwe King, na kama huamini ngoja izinduliwe tarehe 30 Julai Mwanza, harafu ukutane nayo sokoni, pale Majuto anapoamua kwenda kwa mwanaye Jb. |
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi