| Mwigizaji wa muda mrefu wa filamu za Vichekesho nchini Saidi Mohamed 'Mzee Small', amesema kwa sasa hali yake kidogo inaanza kuwa na afadhari baada ya kuanza kuingia Gym kwaajili ya kuchukuwa mazoezi ya viungo vyake ambavyo vimepata kiarusi kutokana na ugonjwa wa presha ya kushuka. Akionyesha picha ya X -ray, ambayo inaonyesha mkono wake wa kushoto ukiwa umeachana kidogo kwa upande wa juu ya bega, pia mguu wakushoto nao ukiwa mzito anabuluza kwa kidogo. Aidha pia amesema kwa sasa maisha yake yanategemea sana, msaada wa watu wanaokuja kumuona. |
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi