Thursday, July 26, 2012

H. Baba na Frola Mvungi harusi yao ni kama Wastara na Sajuki

Mwigizaji wa filamu nchini pamoja na mwanamuziki wa Kizazi kipya Hamisi Ramadhani, hivi karibuni ameamua kuishi mbali kidogo na  mpenzi wake Frola Mvungi kwaajili ya kupumzika kutokana na kuingia kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani. Aidha alipoulizwa kuhusu harusi msanii huyo alisema kwamba yeye na mpenzi wake kwa sasa wanajipanga kwaajili ya kutafuta maisha, hivyo harusi kwao itakuja pole pole tena bila ya kutangazwa sana, kama ilivyokuwa kwa Wastara na Sajuki. Pia alisema kwamba watu wengi wanatamani kujua harusi za wasanii ili waweze kutia maneno mpaka kuvunja ndoa  ya mtu, jambo ambalo yeye kwake anaamini itakuwa tofuti kwani harusi yake itakuwa kimya sana. Aidha alisema kwa sasa yeye na mpenzi wake wameshakamilisha filamu ya MAMA WA KAMBO, na sasa ipo madukani. na kwa muda huu amesimamisha kazi zote za muziki mpaka atakapofungua mwakani.

No comments:

Post a Comment

https://www.facebook.com/gomesamohamedi