Mwandishi wa
filamu ya Super Star ya Wema Sepetu,
Suma Lee amesema uhaba wa fedha
ziliichelewesha filamu hiyo kutoka ingawa aliiandika tangu mwaka 2010 na
kuipitisha kwa wasanii mbalimbali ambao aliamini mwenye uwezo angeweza
kuichukuwa na kuigiza lakini hatmaye ilishindikana kutokana na ghalama
zilizohitajika katika filamu hiyo.
Suma Lee
ambaye ni msanii wa muziki wa kizazi kipya alisema, aliandika filamu tano, na kuanzi kuzipitisha
kwa hao akiwemo mwigizaji Swebe na Nteze
lakini zilishindwa kufanyiwa kazi kutokana na ghalama ambazo msanii ilipaswa
kuzitimiza katika uigizaji mzima wa filamu hiyo.
Aidha alidai
kwamba mtu wa kwanza kumpa tumaini
kwamba angeichukuwa ni Jack Wolper, lakini ilishindikanika baadaye kutokana na
kutingwa na kazi nyingi.
“Jack ndiye
aliyempigia simu Wema na kumwambia kuhusu filamu hiyi, na ndipo akanitafuta kwaajili ya kuiangalia
na kuifanyia kazi” alisema.
Alisema
wakati Wema Sepetu akiigiza filamu yake akiwa na Jacob Stephan ,lakini ikabidi
aisimameshe filamu hiyo na kuiangalia filamu ya Super Star, ambapo aliipenda .
Filamu hiyo
ilianza kubadilishwa vipengele vichache, kwakuwa ilikuwa ni stori ya kiume na
sasa ilibadilishwa mpaka kuwa ya kike.
Ndipo stori
nzima ilianza kufanana na maisha harisi ya Wema mwenyewe, hali ambayo
ilisababisha hata Suma Lee kuchukua kiasi kidogo cha fedha ili filamu hiyo
ikamilike.
|
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi