NYOTA wa muziki wa kizazi kipya kutoka nyumba ya
Vipaji Tanzania ‘THT’ Lameki Ditto ‘Dito’, amesema anatarajia kuachia wimbo wake
mpya wa Niamini, baada ya kumaliza safari zake za nje ya nchi.
Ditto alisema kimya chake kikubwa
tangu alipotoa wimbo wa Tushukuru kwa wote,
ni kutokana na safari kuwa nyingi za kimuziki iliyochukua muda mrefu katika nchi ya
Kenya na Uganda.
Alisema akishatoa wimbo wake huo
ataanza mikakati yake, aliyoipanga kwaajili ya kufanya kazi na wasanii wan je
akianzia na Zambia.
“Nimefungua mtandao wangu kwaajili
ya kusambaza kazi zangu nje, kwakuwa lengo langu sasa ni kufanya kazi na
wasanii wan je|” alisema.
Aliongeza kwa kusema pia kwa sasa amefungua mtandao wake, ambao utakuwa maalumu kwaajili ya kazi zake za kimuziki, na kile ambacho yeye anaamua kukueleza kwa wananchi basi atatumia mtandao huo.
|
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi