| Mwanamuziki Lady Jay Dee amewasili leo saa 7:45 mchana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es salaam akitoka Afrika Kusini katika jiji la Cape Town, alipokuwa akisoma masomo ya muziki ya jukwaani 'Live Band'. Jay Dee alisema hali ya hewa ya Cape Town ni ya baridi sana na nyuzi joto ilifikia 14 C, hali iliyosababisha apate shida kutokana na baridi kuwa kali sana. Mwanamuziki huyo anatajia kupanda jukwaani pamoja na bendi yake ya machozi leo, ili kukumbushia enzi zake kutokana na kuwa nje ya nchi kwa muda mrefu. Jay dee anatarajia kurudi masomoni Januari mwakani. |
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi