Sunday, June 10, 2012

Jide afunguka kuhusu muziki wetu Afrika Kusini

NYOTA wa muziki wa kizazi kipya  na mwanadada aliyediriki kukaa kwenye tasnia ya muziki wa kizazi kipya, kuliko wakinadada wote Judith Wambura maarufu kama Binti Machozi, Komandoo, Jide, Lady Jay Dee na majina mengi zaidi amefunguka baada ya kutua nchini kama wiki hivi kwa kusema  muziki wa Tanzania bado umekuwa  tatizo katika la kutochezwa jingo zetu katika  Media hizo, ikiwemo  Afrika Kusini, ambapo alikuwepo kwenye masomo katika jiji la Cape Town.
Jide  alisema ingawa  Media zetu zimekuwa zikiwaunga mkono kwa kupiga nyimbo zao, kwa wingi lakini nchi hizo zimekuwa hazipi Airtime, nyimbo zetu.
Alisema wakati yupo masomoni  katika jiji hilo,  hakuwahi kusikia nyimbo za Kibongo  katika stesheni yoyote,  zaidi ya wenyewe kwa wenyewe kusikilizishana, kwa kusambaziana Cd. Hata hivyo ameshauri wadau na wasanii wa muziki kuthamini cha kwetu, kwani kitapelekea kufika mbali na watu, kuvithamni baada ya sisi kuthamini cha kwetu.
Jay dee anatarajia kurudi tena masomoni, Januari mwakani ambapo ataenda kumalizia masomo ya muziki wa jukwaani ‘Music Arts Perfomance’ maarufu kama Live band.

No comments:

Post a Comment

https://www.facebook.com/gomesamohamedi