Kundi la
wasanii wa muziki wa kizazi kipya wanatarajia kufanya Tamasha mkoani Mwanza
kwaajili ya kumtafuta msanii chipukizi ambaye atapata nafasi ya kuja kuingia
studio jijini Dar es salaam.
Kundi la
wasanii wa muziki wa kizazi kipya wanatarajia kufanya bonge la tamsha kwaajili
ya kumtafuta mkali wa Mwanza, ambaye watakuja naye Dar es salaam kwaajili ya
kufanya naye kazi zake za muziki akiwa Dar es salaa.

Wanamuziki
hao ambao wakiongozwa na Saidi Fella, alisema tamasha litafanyika mwezi ujao katika viwanja tofauti tofauti ikiwemo tarehe
6 julai, Villa Park,7 Geita ukumbi wa
Ambassador, wakati tarehe 8 watamalizia
katika kiwanja cha CCM Kilumba. Miongoni mwa
wasanii ambao watakuwemo kwenye tamasha hilo ni Ommy Dimpozi, Hamisi Mwijuma
‘Mwana Fa’, Amani Temba ‘Mh Temba’, Hija
Cheka ‘Bibi Cheka’ Ferooz ambaye ataenda kuitambulisha Kibodaboda, H. Number ‘Kasoro
wewe’ na mzee wa Kitorodo ‘Nurudini’ . Wasanii wote wa Tmk pamoja na wasanii wa
Mwanza. “Ni tamasha
ambalo tutachagua msanii bora ambaye tutamsaidia,ili aweze kufika malengo yake ya kimuziki” alisema Fella. Msanii
atakayefanikiwa kufanya vizuri atahamishiwa jijini Dar es salaam kwaajili ya
kazi zake za kimuziki chini ya Mkubwa Fella.
|
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi