| Mwigizaji chipukizi Elizaberth Njau anasema alipenda sana masuala ya urembo, lakini alishindwa kushiriki mashindano hayo kutokana na kuwa na Hipsi kubwa jambo ambalo limemfanya kubaki kuwa kama shabiki wa mashindano hayo. Anadai kwamba kwa mara ya kwanza alionana na kampuni ya Sofia Production, Mkoani Arusha ambapo ndipo anapoishi kwa kusimamia maduka ya dada yake. Kampuni hiyo ilimuomba kufanya naye kazi, na kumwambia afike jijini Dar es salaam. Alikubali kufanya hivyo ingawa aliwasumbua sana katika kukubali kwake kwakuwa alikuwa na mizunguko mingi ya kufuatilia umiss, ila mwisho wa siku akatua jijini. Interview yake ya kwanza, kabla hajaimaliza, Bendi ya Extra Bongo Chini ya Alichoki ikamkubali na kumuomba aonekane kwenye video mpya ya bendi hiyo. Eliza hakukataa, alipomaliza kwenye video ya wimbo huo ndipo msanii Cloud 112 naye alipovutiwa naye na kumvuta kwenye filamu yake ambayo kwa sasa anaanza kuishoot, inaitwa PENZI LA GIZA. Huo ndiyoufupi wa stori yake, kuingia jijini na kuwa Newcomer. Mpokeeni kwakuwa analengo la kufanya mabadiliko makubwa |
Yeah,katika bongo movie dada huyu anayeitwa Elizabeth Njau huenda akawa na jina coz wengi walipomuona katika movie iliyoenda kwa jina la ''PENZI LA GIZA'' amewakonga nyoyo wengi..hata vijijini.big up Eliza!!!
ReplyDelete