Friday, June 29, 2012

Filamu ya Mwalimu Nyerere kuonyesha viwanja vya wazi, Biafra

Mwigizaji wa filamu nchini Stiven Mangele ‘Stive Nyerere’ maarufu kama tajiri mfupi, anatarajia kuizindua kwa mara ya pili filamu yake ya Mwalimu Nyerere katika viwanja vya wazi vya Biafra siku ya jumapili hii.
Anasema lengo lakuonyesha filamu hiyo katika viwanja vya wazi,  kila mmoja apate kuiona na ajifunze maadili ambayo mwalimu alituachia.
Stive alisema kwa hali ya kisiasa ya sasa  watu wanahitajika sana kujifunza maadili ya baba wa taifa, kutokana na na maadili hayo kuporomoka, na ndiyo maana amefikiria kuonyesha bule uwanjani hapo.
Aliongezea lengo la filamu hiyo siyokwambakupata fedha nyingi, ila kuweka histori katika tasnia ya filamu nchini na kumuenzi jemedali huyo wa siasa nchini nchini. Aidhaalidai kwamba kila mmoja atakayefika siku hiyo, hatoondoka hivi hivi bali na  kupata ujumbe uliokusudiwa kwenye filamu hiyo.
“Filamu imeshazinduliwa na imefanya vizuri, lakini ujumbe nahitaji ufike kwa kila mmoja, na ndiyo maana naizindua kwa mara ya pili tena kwa wote” alisema.



No comments:

Post a Comment

https://www.facebook.com/gomesamohamedi