Nyota wa
filamu wa kike nchini Chuchu Hansi Jana alijikuta akiangua kilio kizito baada
ya kuingizwa kwenye jeneza katika ujio wa filamu mpya ya Raula.Katika
filamu hiyo Chuchu ilimbidi aigize kama mtu aliyekufa na kuagwa kwenye jeneza wakati akiandaliwa kwenda
kuzikwa. Kasheshe
ikaja pale alipolala kwenye jeneza, baada na watu kuja kuga mwili wake, ndipo mwanaye kipenzi Faria
ambaye ameigiza kama Star wa movie hiyo na ndiye Raula mwenyewe, alipopita karibu na jeneza hilo huku akilia
kwa uchungu.Raula alilia
kwa hisia kali huku akiita mama!! Mama!!, na kung’ang’amia jemeza huku
akitiririkwa na machozi. Hisia kali
zilipenya maskioni mwa mama yake na kujikuta akiangau kilio kikubwa na
kushindwa kutoka kwenye jeneza hadi aliponyanyuliwa msobemsobe, ili kujaribu kumweka katika hali
ya utulivu. Lakini
tofauti na watu walivyodhani, kwani hali hiyo iliendelea takribani nusu saa
kabla ya kukaa sawa na kurudi tena katika hali yake ya kawaida. Si kwa
chuchu Hansi ambaye mauzauza yalimkuta ila
mwigizaji mwingine, alikutwa na mkasa wa ajabu na kupoteza fahamu papo
hapo wakati akiaga maiti hai ya Chuchu Hansi. Mwigizaji
huyo alipita eneo la karibu na jeneza la Chuchu, akiigiza kulia lakini ghafla
aliregea na kudondoka chini, hali
iliyopelekea watu kwenda kumuokota na kumweka vizuri.
Tofauti
ilivyokuwa kwa Chuchu, kwani mwanamama huyo alipooza kabisa fahamu na kupata
tabu katika upumuaji.
|
| Chuchu akiwa amelala kwenye jeneza,kabla ya kuwekwa pamba |
| Tayari msaraba wake ukiwa tayari pamoja na picha yake. |
| Tayari akiwa ameshawekwa pamba na watu wakipita kwaajili ya kuomboleza kwa kuaga. |
| Kilio sasa kilizidi maradufu |
| Ikafika zamu ya familia yake ambayo aligiza nayo na ndiyo ilikuwa familia yake ukweli, Esha Muheti,akiwa na mwanye Faria 'Raula' |
| Mtoto alilia mpaka akawa mwekunduuu, sauti yake ikapenya kwa mama yake hasa. |
| Ndani ya Jeneza alijikaza kidogo,lakini baada ya kuisha kwa ibada ghafla kilio kikashuka kikubwa. |
| Hapa akiinuliwa na kupelekwa ndani baada ya kuona mambo si mazuri sana |
| Libert akijaribu kumsaidia katika kumpa huduma ya kwanza. |
| Huyu nayealiliampaka akaanza kulegea na hatmaye kuanguka, watu wakajitoa kwenda kumpokea. |
| Alilazwa pembeni kwaajili ya kupata upepo lakini mambo yalikuwa bado. |
| Akabebwa huku na kulekisha akapelekwa kwenye chumba kwaajili ya mapumziko. |
| Wakati huo huo Rachel naye alizidikulia ingawa igizo lilisimamishwa, hadi kichwa kikaanza kumuuma. |
| Hatrmaye ikaandaaliwa chumba kwaajili ya kuwekwa wagonjwa. |
| Ikabidi kutumika nguvu za ziada katika maombi. |
| Shemsa akilia kwa uchungu ingawa igizo liliisha. |
| Hii ilikuwa Part nyingine ya ambaye ilibidi azikwe kabulini. |
| John ilibidi kwanza kuaga, alikuwa muoga kulikokawaida. |
| Aliingia kwenye jeneza huku masharti kibao. |
| Akawekewa pamba, ilifunikwe. |
| Wee!! dakika mbili nyingi akainuka, |
| Familia yake ilikuwa imeshika picha, walikuwa wakimwangalia jinsi alivyokuwa hatulii. |
| Watu makabulini wakaendelea kutizama jinsi filamu inavyoenda |
| Kila kitu kilikuwa tayari bado kufukiwa. |
| Add caption |
| Watu wakamrudisha ndani. |
Inaonekana itashuka bomba. namna hii pre production cast inatoa hisia kali. libeneke bomba kijana.Lukwangule
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteU guyz seem to be keen wit wat ur doing,, kip it up n wishin u ol ze success! we are tuned to wait it..
ReplyDelete