| Nyota wa filamu nchini Stiven Nyerere ameizindua filamu yake ya Mwalimu Nyerere kwa njia ya kutoa msaada katika kituo cha Maunga, kilichopo Ananasif Kinondoni jijini Dar es salaam ilikuenzi jina hilo. Alisema kufanya hivyo ni kama njia ya kumuenzi baba wa Taifa hili, kwani yeye alikuwa akipenda sana watu jambo ambalo anaamini hata yeye akifanya hivyo ni zawadi kubwa wa muasisi huyo. Stiven anasema alipofika Butiama kwa mwalimu, alikuta watu wengi wakiwa na hamu ya kumuona mtu ambaye anaitwa Stive Nyerere jambo ambalo walifurahi sana kumuona. Filamu ya Mwalimu Nyerere inatarajia kuingia sokoni na kampuni ya Steps Entertaiment siku ya ijumaa ya tarehe 26 May. |
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi