| Nyota wa filamu nchini William Mtitu leo alikuwa katika kituo cha Polisi cha Magomeni kwaajili ya kumshitaki mwizi wake aliyemwibia mita ya maji ofisini kwake,lakini baada ya kufika hapo akakutana na Mama bi Amina Omari ambaye naye alikuja kumshitaki William mtitu kwa madai alimtishia mwanye kumvunja miguu kwa kumpiga kwa bastora. Lakini kwa bahati nzuri Mtitu naye alikuwa amekuja hapo ingaswa kwa kesi nyingine, ndipo polisi wakataka kujua zaidi na kila mmoja aliposimulia ikagundulika kwamba bibi huyo alikuwa akimtetea mwanaye ambaye inasadikiwa anamkono wa udokozi na ndiye aliyemwibia Mtitu, Mbao, Mapipa, viti na baadhi ya vitu vingine nyumbani kwake Site. Mtitu mwanzo aliamua kuwachukulia ustaarabu kwa kuwadai kwa polepole kutokana na ujilani mwema, huku akiwaomba kurudisha kila kitu ambacho kiliibiwa. Lakini Bibi huyo aliamua kwenda kwa Serikali za mitaa kwaajili ya kuchukua barua na kwenda polisi kumshitaki Mtitu, ndipo alipokutana napolisi ambao walimshauri kwamba, lazima achague mawili kumleta mwanaye kituo cha polisi mwenyewe, au amshauri arudishe vitu vya watu haraka. Bibi akabaki hoii |
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi