Thursday, May 24, 2012

Cpwaa; nilitumia dola elfu 10 video moja

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Cpwaa amesema kutengeneza video za gharama kwaajili ya kujitangaza katika soko la kimataifa zaidi na wala aangalii maslahi ambayo anayapata kutokana na kazi hiyo. Cpwaa alisema kama video yake mpya ya Mhhh, ambayo kwa sasa inatamba sana katika vituo mbalimbali  vya Tv alitumia dola elfu 10, kwakuwa alisafiri na watu wanne usafari wa ndege wa kwenda na kurudi Afrika Kusini  pamoja na kulala katika Hoteli ambayo pia waliifanyia video hiyo, kuwalipa Mamodal na kukodi vifaa kwaajili ya kuchukulia video. Alisema kwamba watu alioondoka nao hapa ni Meneja wake ambaye ni Mzungu,  Producer wa video Adam Juma wa Next Level pamoja na Produce r wa wimbo huo Luk.

Cpwaa alisema kwa sasa soko la muziki bado kabisa kwakuwa wao wanafanya kazi lakini wanaonufaika ni wachache sana, wao wanabaki kuwatajirisha kama vile makampuni ya Simu na Bia,kwani wanawatumia kuzitangaza bidhaa lakini malipo madogo, huku vitu vingi wakifanya kwa ubabaishaji.

No comments:

Post a Comment

https://www.facebook.com/gomesamohamedi