MSANII Robert Mangwer ‘Ngwear’ amesema kuungana kwa
kundi la Radar Entertaiment ni kufufua vipaji vya wasanii wapya ambao wamekuwa
na kipaji lakini wamwekosa msaada wa kurekodi. Akizungumza
na mwandishi wa safuu hii alisema kampuni hiyo inaundwa na wasanii, Roomy
Jonson ‘Rj’ Kharid Mohamed ‘TID’ Country
Boy na Bobuu wa Kitaa ambao. Alisema kampuni hiyo ya muziki tayari imeshandaa kipindi cha Tv cha Talk Show, ambacho kitakuwa kikizungumzia
mambo mbalimbali ya wasanii pamoja na matukio ya show mbalimbali.
“Lengo letu
kwa sasa ni kuitambulisha kampuni watu waijue, kisha ndipo tuanze mikakati ya
kuinua vipaji vipya ambavyo vimekosa msaada katika muziki” alisema.
Kundi la Radar
tayari limeshakamilisha albamu moja, na hivi sasa wanatarajia kuachia wimbo
Tunakiki alioshiriki Tid na Ngwea.
|