| Mwigizaji maarufu wa filamu nchini Richie Rich, hivi sasa amejipanga katika ujio wa filamu yake mpya ya Uyoga,ambayo amekutanisha warembo ambao huenda hujawahi kuwaona katika filamu yoyote. Nifilamu ambayo kwangu mimi natamani sana sikumoja nije kuiona, maana wamejaa wasanii ambao wengi ni wale wanaochipukia na kutokea sehemu mbali mbali kama Miss Kinondoni mwaka 2011 Stera na Miss Arusha mwaka 2011 Aisha. Pia nimekutana na watu ambao huwa napenda sana kuona kazi zao kama Seleman Barafu, Hatman, Recho na Libert. |