Lile nguli la filamu za kuchekesha Tanzania, Athuman
Majuto ‘ King Majuto’, hivi karibuni aliingia mkataba na wauzaji wa bidhaa za Azam, na kumchukuwa akiwa kama Balozi mpya wa bidhaa hizo huku akishirikiana na Hussein Kiety 'Sharo milionea' katika kazi zake. Majuto alisema mkataba na kampuni ya Al – riyami ameuvunja kwa kuwalipa shilingi milioni 20. Alisema kampuni ya Al - riyami kwa sasa imekuwa inarusha kipindi cha
Vituko Show zile ambazo aliigiza zamani wakati yupo nao.
“Sasa hivi
kazi zote nitakuwa nikizifanya kwaajili ya bidhaa za Azam, pia nipo kwenye
mikakati mingi juu ya kazi zangu mpya” alisema.
Hata hivyo
King Majuto kwa sasa kazi zake atakuwa akifanya Dar es salaam na akimaliza
anarudi Tanga ambapo kazi zake zingine zinaendelea, wakati huo huo katika kampuni hiyo anaenda kukutana na mzee Small ambaye amekuwa akitangaza bidhaa za kampuni ya Azam kama vile tui la nazi katika bidhaa ya Azam.
|