| Mwigizaji maarufu wa filamu za kuchekesha nchini Mzee Small leo ameanguka ghafla na kukimbizwa katika hospitali ya Amana iliyopo wilaya ya Ilala. Chanzo cha kuanguka kwake na kulazwa katika hospitali hiyo inasadikiwa kuwa ni ugonjwa wa presha ambao ulimuanza ghafla na kujikuta akizidiwa na kuanguka na ndipo ndugu jamaa waliokuwepo hapoa walipomkimbiza katika hospitali hiyo. |