| Lile gwiji la filamu za kuchekesha nchini King Majuto ameeleza kwamba leo alikuwa Dar es salaam kwaajili ya kufuatilia vifaa vya gari lake, pia kufuatilia fedha ambayo anaidai Grobal Publishes watengenezaji wa gazeti la Risasi, kwa kuwa walimwahidi fedha baada ya kushinda katika tuzo za Risasi Award mwaka 2011 na mwaka 2012 lakini wamekuwa wakimzungusha kila siku. King Majuto amesema kwamba waandaji hao anapowafuata wanamjibu kwamba wao hawahusiki katika tuzo hizo, ila ni wategeneza wa gazeti ndiyo wanahusika bila ya kampuni ya Grobal kuingilia. Hapo ndipo unapokuja mshangao kwamba itawezekana vipi watu waandae tuzo za kampuni bila ya kampuni yenyewe kuhusika na kama sio ubabaishaji. Pia Majuto ameleeza kwamba waandaaji wengi wa tuzo wamekuwa wababaishaji, kwani hadi hivi sasa anadai fedha kibao kutoka kwa waandaaji mbalimbali wa tuzo, bila ya kujali umbali ambao anatoka na fedha anazotumia huku akiwa na familia, wakati pia fedha zenyewe ni shilingi elfu 30. Pia ametoa ushauri kwa waandaji wa tuzo mbalimbali ni bora kuwapa wasanii tuzo za maana au vifaa vya kazi kuliko kuwapa mavyuma ambayo kwa muda mfupi yanachakaa na kushika kutu ovyo. Miongoni mwa watu ambao anawadai na wanamzungusha pia wamo tuzo za muziki Tanzania... Jambo hili anasema linawavunja moyo kwakuwa wao wanatumiwa huku manufaa wakiyapata wachache sana kwa ujanja ujanja. |