|
Uzinduzi wa Documentary ya mwanamuziki
wa Bongo Fleva Cyril umeanza kuingia nuksi baada ya Baraza la Sanaa Tanzania ‘BASATA’
kumtumia barua ya kuomba atoe maelezo kwaana kwamba msanii huyo sio mtanzania
ila ni Mkenya.
Jambo hilo limemshangaza sana msanii
huyo kwa madai kwamba yeye ni Mtanzania harisi, na wala hayo ambayo anaamibiwa
yeye hayajui.
“ eti wanasema NIMETENGENEZA
skendo...huu ndio uthibitisho namba 1,namba 2 ni mazungumzo ya simu baina yangu
na bosi wa BASATA leo mkuu Bwana LUHALA yalio rekodiwa” alisema msanii huyo
baada ya watu kuhisi huenda kufanya hivyoni kujipigia chapuo ili afanye vizuri
kwenye uzinduzi huo.
Lakini Cyril alisema ingawa alitumiwa
barua hiyo, lakini kwake bado hajasitisha suala la uzinduzi wa Documentary hiyo
pale Maisha Klabu siku ya leo jumapili, kwakuwa yeye ni Mtanzania harisi. |