Sunday, May 13, 2012

Mamiss 2006, na kashfa zao

Mamiss Tanzania mwaka 2006 - 2007 wamekuwa wakiliteka jiji huenda kuliko msimu wowote wa Mamiss ambao umewahi kupita katika nchi hii. Huenda haitatokea tena mamiss ambao wenye mbwembwe, ushindani, majigambo, ubabe, na wenye vituko kama msimu wa 2006 kwenda 2007. Kila mmoja alipart kwa wakati wake kama Movie, ili kuonyesha kwamba yeye anaweza,  hawa ndiyo wamekuwa vinara kwenye magazeti na kufanya jiji lichangamke kwa mambo yao, tofauti na nchi za wenzetu ambapo wanamuziki huwa na vituko zaidi kama ilivyo kwa Beyonce, Nick Minaj, J.L, Witney wiston, Rihanna na wengine ambao wanaleta raha na karaha kwenye miji yao. Hapa kwetu kama ilivyo  kwa cheo chake, tunaye Miss wa wa kwanza  Tanzania mwaka 2006 - 2007 Wema Sepetu bingwa wa Skendo, pia wakafuata wengine... ambao wote walikutana jukwaa moja mwaka mmoja.
Lisa Jensen yeye aliibuka mshindi wa pili Miss Tanzania 2006,naye aliguswa na skendo ingawa si sana, na aliweza kukwepa skendo zaidi zinakuwa zikimnyemelea hasa baada ya kujaribu kutia kwato zake kwenye Bongo Movie.
Miss Tanzania namba 3 mwaka 2006, Joketi 'Kidoti' yeye alifanikiwa kuzikwepa skendo kwa muda mrefu kwakuwa watu waliamini ni mcha mungu na alitulizana kwenye mitindo, balaa lilipofika mwaka 2011 mwishoni, alianza kwa kuimba kama wimbo wa King and Queen ya Ay na baadaye kuwa Presenter wa Channel O,  lakini mwaka  2012 ni mmoja wa watuhumiwa wa skendo ambazo zimemweka wazi  kwenye Diamond party iliyofanyika mlimani City.
Huyu naye likuwa miongoni mwa washiriki wa miss Tanzania mwaka 2006, skendo yeye alikuwa nazo za  tangu siku ya kwanza alipoingia kwenye tasnia ya filamu na kuwa bonge la msanii, lakini  zilizidi pindi alipoolewa na Ndikumanya.
Kama ilivyokuwa kwa Wema Sepetu na kwa Aunt Ezekiel nayo imekuwa hivyo hivyo, kila kukichwa watu wanamuonyeshea kidole, tangu alipoanza kujulikana kwenye tasnia ya filamu nchini.Hivi ni kweli watu wanachosema mamiss wa 2006 walipatwa na pepo mchavu?