Wednesday, May 16, 2012

Pengo laKanumba ndani ya God Kingdom ya Pastor Myamba.

Mwigizaji maarufu wa filamu nchini Pastor Myamba anatarajia kuachia filamu yake mpya ya God Kingdom, ambayo itakuja kueleza nguvu za mungu, baada ya ile ya Devil Kingdom ya marehemu Steven Kanumba kuelezea nguvu za shetani. Myamba alisema katika filamu hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa sana marehemu Kanumba alionyesha mchango wake ili kukamilika kwa filamu hiyo, ambayo pia ilibidi aigize. Myamba alisema pengo la Kanumba limeendelea kuwa kubwa kwakuwa hakuna ambaye anaweza kuijaza nafasi ya mwigizaji huyo, na hatmaye ameamua kuwachukuwa wasanii mbalimbali ambao waliigiza katika Devil Kingdom, ili kuleta uharisi wa filamu hiyo. Alisema miongoni mwa wasanii ambao aliwachukua ni Patcho Mwamba,ambaye alikuwa mshirika wa karibu sana na marehemu Kanumba. (Picha; Patcho Mwamba akiwa na Meya pamoja na Mogani)
Filamu ya God Kigdom ikiendelea kushootiwa
Miongoni mwa watu ambao walikuwa wakifanya kazi ya karibu na Kanumba ni Mzee Jengua ambaye naye ameg'ara vizuri kwenye God Kingdom ni Mohamedi Fungafunga 'Jengua'  hapa akiwa na Joyce Haule.
Wanafunzi wa chuo cha Tanzania Film Trainning Center (TFTC), wakiendelea kushoot kwaajili ya kupata uzoefu zaidi
Emmanuel Myamba 'Pastor Myamba'akiendelewa kufanyiwa Make Up, kwaajili ya kuingia mzigoni.
Wanafunzi wakiendelea kufanya kazi
Mwigizaji maarufu na wazamani sana Zawadi, kwa sasa naye ni mwanafunzi wa chuo hicho kwaajili ya kwenda kiujuzi na kielimu katika tasnia ya sasa ambayo inahitaji ubunifu.
 Hii ndiyo Devil Kingdom ya marehemu Steven Kanumba akiwa na Ramsey