Sunday, May 20, 2012

Uzinduzi wa filamu ya TOBA, waweka histori Zanzibar

Uzinduzi wa filamu  ya TOBA katika ukumbi wa Safari Hall uliopo Bwawani katika mji wa Zanzibar umeonyesha wazi jinsi watu wa Zanzibar wanavyomkubali msanii  Issa Mussa  'Cloud 112' , na kumjengea tumaini msanii huyo katika  mji aliozaliwa. Uzinduzi huo ambao mgeni rasmi ni Makamu wa raisi wa kwanza Zanzibar Maalim Sefu sharifu Hamadi (wa katikakati), pia uliudhuliwa na viongozi mbalimbali wa  serikali ya Mapinduzi Zanzibar akiwemo,  Spika wa baraza la wawakilishi Zanzibar Mh Pandu Ameir Kificho(Kushoto aliyevaa kanzu nyeupe), waziri wa Utamaduni na michezo Zanzibar Said Ali Mbarouk, mkuu wa mkoa mjini magharibi na wengine wengi.  Wananchi wa mjini Zanzibar waliudhulia kwa wingi kiasi cha kupelekea kuisha hadi tiketi za ziada, hali ambayo ilisababisha ukumbi kujaa, na wengine kubaki nje kwa kukosa tiketi sababu  ndani kulijaa sana. Pia katika uzinduzi huo Cd za filamu ya TOBA , ziliuzwa kwa mnada huku Waziri wa utamaduni na michezo pamoja na mama Loraa walinunua parti 1 & 2 kwa shilingi laki 2. Cd zingine ziliuzwa kwa laki moja, elfu 50, elfu 20 na zingine zikauzwa kwa shiling 10000na 5000,ambapo zikaisha zote. Maalim Sefu alisema tukio hilo litabaki katika histori  kwakuwa hakuwahi kuona ukumbi wa Safari Hall ukijaa kama ulivyo jaa, ila alimshauri  Cloud 112 na wasanii wengine kwamba, watakapohitaji  kufanya tukio lingine kama hilo, basi waombenafasi ya uwanja wa kutosha.
Wema Sepetu, Jocob Stephan 'Jb' na Hatman Mbilinyi wakielekea kwenye uzinduzi wa filamu ya Toba.
Moe One nikiwa na Pacha wa Cloud 112, yeye anaitwa Kharifani. Kuonyesha siku hiyo ilijaa bahati na baraka. Pacha wa Cloud 112, mkewe alijifungua mtoto wa kike muda wa saa sita za usiku wakati tamasha linakaribia kuisha jambo ambalo liliongeza faraja kwa familia ya Cloud.
Filamu mbalimbali za Cloud 112 zilitangazwa usiku huo
Huu ndio ukumbi wa Safari uliozinduliwa filamu hiyo kwa nje kabla ya watu kuanza kuja.
Ukumbi kwa ndani wakati watu wakiendelea kupamba
Shekh Steven Nyerere akiwa ndani ya kanzu
Mwakilishi toka Step Entertaiment ambao ndiyo wanaoiwezesha filamu hiyo kuingia mtaani.
Wema Sepetu akiwa na Jb ndani ya pozi
Irene Uwoya akifuatilia mawaidha kwa umakini
Mambo ya ustaarabu wa pwani, vitezo vya udi na maji ya karafuu full kunukia,
Watu kibao walibaki nje lakini wakiwa na tumaini la kuingia, jambo ambalo lilibaki kuwa tumaini kwani nafasi ndani zilijaa kiasi cha watu hawa kutoingia ndani. Ila walinunua Cd ya filamu ya TOBA.
Madrasat ya Home,
Kulia ni mama Lora ambaye alinunua Cd mbili ya Part 1 & 2 ya filamu ya TOBA kwa njia ya mnada kwa shilingi laki 2.
Aliyeigiza kama kimada wa Yasir, katika filamu ya TOBA naye alikuwepo katika uzinduzi huo.
Madrasat mbalimbali zilikusanyika kwaajili ya kutoa burudani yenye msimamo wa kidini.
Hivi ndivyo watu ndani walivyojazana kiasi cha watu kusimama wakati ilitakiwa uwe uzinduzi wa kukaa kwenye kiti.
Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambao wamekaa kwenye viti na Cloud 112 na waliosimama ni wasanii ambao wamekuja kumuunga mkono msanii mwenzao.
Cloud 112 akiwa na ndugu zake huko Visiwa vya karafuu

Waziri wa uatamaduni na michezo, akiwa ametulia alinunua Cd ya Toba part 1&2 kwa shiling laki 2
Familia yote ya Cloud 112 ambayo ikifurahi kwa kupata mtoto na kuzindua filamu kwa kisindo.
Makamu wa kwanza wa Zanzibar maalim Sefu Sharifu Hamad akizindua filamu ya TOBA, kwa mara ya kwanza.
Maalim Sefu Sharifu Hamadi Akikabidhiwa filamu ya TOBA part 1&2 na Issa Mussa 'Cloud 112' mwigizaji, Muongozaji na mtungaji kutoka kampuni ya CY & CL Company, walioitengeneza filamu ya TOBA.