Sunday, April 29, 2012

Uzinduzi Respect Nyerere waja kwa mbwembwe

NYOTA wa filamu  Stive   Nyerere amesema  katika filamu yake ya Respect Nyerere ameigiza  mwanasiasa na kiongozi mkubwa wa hapa  ilikuvuta taswira mpya katika tasnia ya filamu. Stive ambaye ameungana na Mainda katika kampuni moja ya The Nyerere Power, amesema kwamba  mwanasiasa huyo ambaye anaamini siku ya uzinduzi  wa filamu hiyo  anatarajia atakuwepo  ‘Surprise’. Alisema kufanya hivyokwakuwa baba wa taifa  mwalimu Nyerere alikuwa kipenzi cha Watanzania wengi. Hivyo uzinduzi wa filamu hiyo anatarajia kuufanya  katika viwanja vya Leaders Club ilikutoa nafasi kwa kila mmoja kuiona. “Nipo kwenye mikakati ya mwisho katika kukamilisha uzinduzi huu, kwakuwa nataka uwe wa kipee na wakuigwa” alisema.
Pia kutazinduliwa na filamu yake nyingine ya  Mke mwema, na baada ya hapo ataenda Zanzibar kwaajili ya filamu ya Ilove You Zanzibar.
Stive Nyerere akiigiza kama mwalimu akiwa katika Zizi la Ng'ombe Butiama.
Bi Mwenda akiigiza kama mama Maria Nyerere, wakiwa Butiama
Filamu mpya ambayo inatarajiwa kuzinduliwa pamoja na filamu ya Respect Nyerere, inaitwa Mke mwemaikiwa imeandaliwa na Tne Nyerere Power chini ya Mainda na Stive Nyerere.
Kama unataka kuujua ukatuni wa Stive Nyerere angalia kwenye filamu hii, hapo ndipo utakaposhika mbavu mkononi.