WANAJAMII
wametakiwa kutumia kazi za sanaa za mikono za wasanii wa hapa nchini katika
kupamba nyumba zao ili kuongeza hamasa na maendeleo ya tasnia hiyo hapa nchini.
Wito huo
ulitolewa juzi na Mdau wa sanaa za uchoraji Candida Bahame ambae ni Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya Nyayo Za Mama wakati akizindua maoenesho ya wiki mbili
ya kazi zake za sanaa.
Candida
alisema kuwa wasanii wa hapa nchini wanao uwezo wa kuchora na kutengeneza picha
kwa kutumia viashiria mbalimbali vya kisanii ambavyo zinapendezesha nyumba.
|