Sunday, April 29, 2012

Aunt kuungana na Mboto

NYOTA  wa filamu Aunt Ezekiel  amesema  filamu  ya Siri Sirini itakayotoka hivi karibuni huenda ikasababisha kuundwa  kwa kampuni mpya ya utengeneza jiwa filamu nchini akishirikiana Haji Salum ‘Mboto’.    Aunt amesema amekuwa mara nyingin  wakifanya kazi kwa pamoja na Mboto, hadi kupelekea kuingia kwenye  mazungumzo ya kuunda kampuni baada ya kuitumiakampuni anayomiliki Aunt sasa hivi. Aidha alisema kwamba filamu hii wakiikamilisha itakuwa ni ya  tatu, baada ya zilizotoka filamu ya   Mke mwema, House boy & girl  na sasa hivi hii  Siri Sirini na wakatihuo wakijiandaa na filamu ya Radio Presenter.  “Pia tupo katika kujadili kama tuendelee kutengeneza filamu za kuchekesha au tubadilike na filamu makini” alisema Aunt.  Alimalizia kwa kusema kwamba  filamu zao wanategemea sana maoni kutoka kwa wadau na mashabiki wao.