BENDI ya ya Five Star Modern Taarab inatarajia kuingia
kambini katika kuandaa albamu ya pili
tangu ilipopata ajali na kupoteza wanamuziki wake. Kiongozi wa bendi hiyo Ally Juma ‘Ally Jay’ ,
alisema albamu hiyo itakuwa ya pili baada ya ile ya Riziki mwanzo wa Chuki,
ambayo itabeba nyimbo tano hadi sita.
Alizitaja
baadhi ya nyimbo ambazo zitakuwepo ni kusema
mtasema vibaya kutukanana, Silipizi kwa ubaya,
na nyingine ambazo tayari na zingine zinatengenezwa studio. “Mashabiki
wa Five Stars naomba waendelee kuifuatilia bendi yao kama zamani, ili waweze
kujua nini tunatajka kukifanya” alisema
Bendi ya
Five Stars Modern taarabu ilipoteza wasanii wake 13 katika ajali iliyotokea
Morogoro mwaka jana March na kumpoteza mwimbaji wake mahaili Issa Kijoti.
|