Saturday, April 14, 2012

Bob Junior ajitoa kwenye mzozo

Mwanamuziki wa kizazi kipya ambaye kwa sasa anatamba na video ya wimbo wa Nichum, Bob Junior amesema maelezo yaliyoandikwa na magazeti la hivi karibuni ya udaku ni uongongo mtupu. Amesema magazeti kwa sasa yamekuwa yakihaha katika kutafuta stori,kiasi cha kuzusha uongo mwingi mpaka kuchanganya wasomaji. Amesema yeye hakumpigia simu katika usiku huo, na maneno ya magazeti hayo wameyapata wapi?. "Sihusiki na upuuzi wa magazeti haya kwa kile wanachokiandika" alisema. Bob Junior alisema kwamba mtu kumshirikisha katika video ya muziki 'Nichum' ni jambo la kawaida, mbona wengi wamefanya hivyo.