| Bibi Cheka anatarajia kufanya bonge la Tamasha katika ukumbi wa Jamuhuri Mkoani Morogoro, mwanamuziki huyo amesema kwamba hii itakuwa mara yake ya kwanza, kwakuwa aliwahi kupanda jukwaani katika Media Day kwakuwa alikuwepo sehemu ya tukio na kulazimishwa kufanya hivyo. Amesema lakini siku ya Pasaka anatarajia kufanya kazi ya maana kwakuwa ndiyo siku yake ya kufanya Show kwa mara ya kwanza. Miongoni mwa wasanii watakao msindikiza ni Dogo Aslay, Mhe Tembana wasanii kibao. Pia zawadi zitakazotolewa kwa mtoto atakayeimba vizuri wimbo wa Naenda kusema, atapata Tv na wengine wataondoka na zawadi kibao ikiwemo begi pamoja na madaftari yake. |