Saturday, April 21, 2012

Badibakule amfuata Muumini Twanga Pepeta

Mwanamuziki  Badibakule kutoka nyanda za kusikini  na kuibuka kwa  mara ya kwanza katika bendi ya African Revorution ‘Wanatamatama’ na kutamba  na nyimbokama ‘Nipishe’ chini Mwijuma Muumini hivi sasa  ameungana na kiongozi wake huyo wa zamani katika bendi ya bendi ya African Stars ‘Twana Pepeta’. Badibakule anasema kwake ni kama sehemu ya kurudisha jina lake  ambalolimepotea ingawa siku zote bado yupo kwenye bendi. Alisema kufanya kazi na bendi hiyo, si jambo geni kwake kwakuwa hata African Revolution, iliyomtambulisha kwenye muziki ilikuwa chini ya Asha Baraka na sasa hivi yupo tena chini ya huyo huyo. Mwanamuziki huyo kwa miaka kadhaa alikuwa katika bendi ya  T.OT Plus na baadaye kujiunga na  Lavent Music ya Morogoro. Katika bendi yake ya Morogoro alikaa kwa muda wa miezi minne, na jumaanne ya April 18 ndipo akajiunga rasmi na bendi  ya Twanga. Anasema alipojiunga na bendi hiyo alifanya tamasha lake la kwanza, katika viwanja vya Club Bilicanas siku ya juma tano, kwasasa  anatarajia kufanya tena  tamasha katika viwanja vya Leaders Club juma mosi. Hata hivyo alisema kwamba hajasaini mkataba wowote, ila wamekubaliana kwa njia ya mdomo, huku akiendelea na kazi.
Pia kiongozi wa bendi hiyo Hassan Rehani, alisema kwamba mikataba ya wachezaji mpira ndiyo mara nyingi imekuwa ikiheshimiwa, lakini ya wanamuziki imekuwa tofauti sana. Kiasi cha kutoitilia mkazo kwakuwa hata wanapowasainisha, basi wanamuziki hao wanapoamua wanaondoka na ndiyo maana wanatumia makabaliano ya mdomo.