Thursday, April 19, 2012

Swahili Hip hop Family,Okwi na Lamar wetembelea watoto watukutu

Kundi la ASAR Entertaiment 'Swahili Hip Hop Family' leo wametembelea katika mahabusu iliyopo jijini Dar es salaam inayotunzo watoto wenye tuhuma mbalimbali, ambao wapo chini ya umri wa miaka 18
Ilitembelea katika sero hiyo, kwaajili ya kuwapa moyo watoto hao, na wasikate tamaa kutokana na tuhuma mbalimbali ambazo zinawakabili.
Pia kiongozi wa kundi hilo Imam Abass, akiongozana na mtayarishaji wa muziki kutoka Fish Crub Record, Lamar mchezaji wa Simba Emmanuel Okwi na Amir Mafutaa.
Wasanii mbalimbali wa muziki kutoka Arusha na Dar es salaam nao walikuwepo, pamoja na wachoraji kwaajili ya kutoa elimu kwa watotohao.
Kiongozi wa kituo hicho Alex Bwile, alisema ingawa watoto wengi wanaofikishwa hapo, wamekuwa wanakabiliwa na kesi ya wizi, ubakaji, ukabaji,na mauaji.
aidha amedai kwamba watuhumiwa wengi wanaowasilishwa hapo, ni wale wa matukio ya wizi lakini wakiwa na umri wa chini ya miaka 18.
Hadi wakati wanapeleka vitu hivyo watoto waliokuwa wakituhumiwa kwa kesi za mauaji ni wawili, na mmbakaji mmoja na wengine ambao ni wiwengi wanatuhumiwa kwa wizi.
Baadhi ya watotowengi kati ya hao wametoka Arusha, na wengine Mbeya.