Mmiliki wa chuo cha Tanzania Film Tranning Center ‘TFTC’ na mwigizaji Emmanuel Myamba wasanii mbalimbali tayari wameshajitokeza katika kuchukuwa wanafunzi ambao wamemaliza muhura wa kwanza katika chuo hicho. Myamba amesema wanafunzi hao kwa sasa wapo katika mafunzo ya Vitendo maarufu kama Field, tayari wasanii wakubwa kama Steven Kanumba, Vicenti Kigozi ‘Ray’ na Jacob Stephan ‘Jb’ wameshakuja kuwahitaji. Lakini Myamba amesema wasanii hao kwa sasa wanaigiza filamu za chuo, ikiwemo Zero Brain, Lost Sound na zingine. |