Thursday, March 1, 2012

Omari Mkali bado hajaijua dini yake

Mwanamuziki ambaye alitikisa katika miondoko ya mduara nchi, katika bendi ya Chuchu Sound ambaye ilitisha pale walipoweka vionjo kama 'Bwana chuchu unataka pilau'....., Omari Mkali, bado yupo njia panda katika usahihi wa dini yake. Alipokutana na  uso kwa uso na BONGO UNIT,  alisema  anaabudu mungu na aangalia dini. Alisema hali hiyo inatokana na mama yake kuwa mkristo na baba yake kuwa muislam, na yeye kubaki njia panda. Muda mwingi anashinda na  Biblia na Qur-an ,  zote anapozisoma ndipo anapopata uamuzi wa kumuimbia mungu bila ya kufungamana upande wowote. lakini katika kuchokoa chokoa hapa na pale, ndipo aliposema aliwahi kumwambia mwanamuziki mwenzake, aangalie maisha ya awali kipindi wanaanzisha bendi, na hali ya sasa ni wapi wanakwenda,  hivyo amechoka kuwaimbia watu kwenye mabaa na hamna lolote analopata, na kuamua kujitupa kwenye injili huenda kuna chochote atakachopata. Omari mkali pia alisema zaidi ya nyimbo zake mbili kuwemo kwenye albamu ya pamoja Mkono wa Baba akiwemo na Stara Thomas na wengine,  pia anajiandaa  na albamu yake mwenyewe.