Friday, March 2, 2012

Mr Nice aja na utamu mpya


Mkali wa staili ya TAKEU,  Lucas Mkenda ‘Mr Nice’ amewaambia mashabiki wake kwamba  kwa sasa yupo kwenye  utawala mpya ‘Management’ ambayo  itasimamia katika kuifufua staili ya TAKEU.
Mr Nice alisema kwamba  mara kwanza aliweza kukosea sababu alikuwa akifanya kazi zake bila ya Meneja, lakini sasa yupo kkwa meneja mpya ambaye atamuongoza katika video yake anayoifanya leo.
Alisema video hiyo huenda ikawa kali kuliko zile zilizopita, kwakuwa hizi anafanya akiwa na ujuzi zaidi huku soko la muziki likiwa limetanuka zaidi. Hizi sasa zinasimamiwa na Duke pamoja na mkali Lamar 'Ahaaaaaaaaaaaa' toka Fish Crub Record