| Kundi la Tmk Wanaume Family chini ya Mkubwa Fella, pembeni wakiwemo Chege na Temba huku kati pakiongozwa na Dogo Aslay wote kwa pamoja wanaungana na kufanya Party moja inayotambulika kama Tmk Wanaume Family Party siku ya juma mosi katika ukumbi wa Times Square pande za Mbezi ya Kimara. Mkubwa Fella amesema katika tamsha hilo Dogo Aslay ataongoza kundi la Mkubwa na Wanawe, lakini kwa upande wa Tmk Wanaume Family kutaongoza na Temba pamoja na Chege. hata hivyo kikosi kizima cha wasanii wote wanaounda makundi hayo mawili, siku hiyo watakuwepo pamoja katika kuonyesha uwezo wao. Mkono mmoja weka juu, Kichwa kinauma na kali zingine kama hizo zinatakuja kuleta maujanja.... |
|