Bnei ya msondo ngoma, chini ya kiongozi wao Saidi Kibiriti, amesema kumchukuwa mwanamuziki Shaban Land katika bendi ya Sikinde sio kuikomoa bendi hiyo ila walikuwa na tatizo la mpiga Saxophone. Kibiriti alisema albamu yao ya Suruhu ilichelewa kutoka kwa sababu ya mpigaji wa kifaa hicho ambacho hapa nchini wapo wachache sana. Alisema hali hiyo ilibidi wamchukue mpigaji huyo kwakuwa walikuwa hawana njia nyingine, iliwaweze kuendelea kukamilisha nyimbo sita walizozisiamamisha. |