| Mwanamuziki kutoka pande za South Afrika wanaopahita bondeni, jana amekuja na kiloja cha aina yake.Kwanza mlinzi wake, alikuja akiwa amevaa kininja usoni na plasta mdomoni,harafu alikuwa akionekana kama mtu anayetafuna bazoka jambo ambalo nikama la kustaajabisha na hata waandishi walipomuomba afunue uso japo kidogo aligoma. Pia kwa D j Cleo mwenyewe,ambaye ndiye kusudio la wapenzi wengi wa muziki wa kwaito, kumuona leo katika viwanja vya Posta,aligoma kabisa kutoa Freestyle ya wimbo wake wa Facebook, ambao umekuwa gumzo. Hata hivyo alisema mambo yote yatakuwa pale viwanja vya posta... Ila kwa Ommy Dimponzi mtoto wa hapahapa kwetu Dar es salaam anayewakondesha watu kwa wimbo wake wa Ng'aing'ai, yeye alimwaga mashairi ndipo ajabu nyingine ikatokea pale Dj Cleo na wapambe wake walipoanza kucheza na kuimba wimbo huoo.. |