| Bendi ya Twanga Pepeta chini ya mkurugenzi Mama Asha Baraka, inatarajia kumtafuta Model katika usiku wa leo pale Club Billcanas katika usiku wa Out Africa Night. Bendi hiyo imesema Models hao watakuwa wakionyesha mbwembwe zao, huku wakitoa offer kwa wale ambao watakuja kuwachukua kwaajili ya matumizi mbalimbali kama filamu na matangazo mengine. Pia Bendi hiyo inatarajia kufanya Tour ya kwenda Lindi na Mtwala kati ya siku ya Ijumaa na Jumamosi kwaajili ya kuitangaza albamu yao ya Dunia Daraja. |