Wednesday, February 29, 2012

Jinikabula anaogopa kuchezewa kwenye filamu

Mwigizaji aliyevuma kwenye tamthiria ya Jumba la Dhahabu, amesema kukaa kwake kimya kwa muda mrefu ni kutokana na kuogopa kucheza katika filamu za kibongo pasipo maslahi. Muigizaji huyo mwenye mbwembwe za aina yake, amesema msanii anaweza kucheza filamu na kulipwa kiasi kidogo kisa ushikaji, tofauti na kile ambacho amewainingizia wasanii hao. Pia amesema yeye ni muigizaji aliyekamilika, hivyo haingii kwenye tasnia ya filamu kwaajili ya kufuata wanaume, na kuwaambia wasichana wenzake wanaofanya hivyo waachane nayo kwani sanaa ni kazi kama kazi zingine.