Akiongea katika uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam, Steve alisema kampeni hiyo kwaajili ya kuwavesha viatu wanaufunzi wa shule za msingi hapa nchini.
Alisema katika kampeni hiyo wamefanikiwa kukusanya zaidi ya jozi 450 za viatu kutoka katika taasisi mbalimbali ambapo Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania ( TPA) waliochangia Sh Milioni 65.9.
" Tunatarajia kuzunguka nchi nzima kuhakikisha tunawavisha watoto viatu sisi wenyewe.
Katika kampeni hii tutashirikiana na wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya pamoja na shule za msingi" alisema
Mwakilishi wa mkurugenzi mkuu wa TPA, Beatrice Jairo alisema wameunga mkono taasisi hiyo kwakuwa wamekuwa na kawaida ya kutenga fungu kidogo kwaajili ya kuwarudishia wananchi kwa kile walichokipata
Alisema tayari kila kitu kimekamilika ambapo wanatarajia kuanza muda wowote ila wataanza na Zanzibar.
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi