Wednesday, September 7, 2022

Mashindo ya Gofu Afrika kwa mara ya kwanza yafanyika Tanzania



RAIS wa Chama Cha Gofu Wanawake Tanzania (TLGU) Sophia  Viggo  amesema wanatarajia kutoa zawadi kwa nchi 12 kati ya nchi 21 za  Afrika   zilizoshiriki katika mashindano ya mpira wa Gofu Wanawake  Afrika ‘All Africa Challenge Trophy’   (AAT) yaliyofanyika hapa nchini.

 alisema mashindano hayo yalianza Septemba 6 katika viwanja vya GymKhana jijini Dar es Salaam,  ambapo yamechukua siku tatu yakihusisha nchini wanachama kutoka Afrika ikiwemo Uganda, Kenya, Nigeria na zingine.

Alisema  kwa mara ya kwanza Tanzania inaandaa  mashindano ya Gofu Afrika ,  yanayofanyika kila  baada ya miaka miwili na kuudhuliwa na  nchi 21 huku zingine zikishindwa kuudhulia kutoka na changamoto mbalimbali ambapo zipo zilizokosa viza  zipo  zilizokubwa na  mafuliko na zingine  kocha kufika ila wachezaji kutowasili.



“Matarajio yetu wageni wafurahi, lakini pia tufanye vizuri kwakuwa tumeanza  vizuri na tunamaliza vizuri”

Wakati huo huo rais wa mpira wa Gofu wanawake kutoka nchini Nigeria, Julieth  alisema hii ni mara ya kwanza  kufika nchini Tanzania,  ambapo amekuja kwaajili ya mashindano ya Gofu Afrika.

“Nimefurahi kufika Tanzania, nimefurahi jinsi walivyoandaa tamasha, nimependa vyakkula vya Kitanzania lakini pia nimefurahi jinsi walivyotupokea kuanzia uwanja wa ndege mpaka hotelini ambapo mazingira ni mazuri na yakirafiki” alisemaa.


 


No comments:

Post a Comment

https://www.facebook.com/gomesamohamedi