Jina lake Halisi anaitwa Shaibu Hassan ambaye anatambulika kama Badist Mbwa Mzee kiongozi wa kundi la Wahuni la Machawa Camp ambalo linapatikana Mabibo Makutano.
Badist ni kijana kama vijana wengine ambao wanaamini kwamba sifa pekee ya kujulikana mtaani ni kuwa muhuni wa kupindukia na kuogopwa na kila mtu
Akiwa katika harakati za kujipa utawala katika maeneo ya Mabibo Makutano, ndani ya Tamthilia ya Mabibo Mabwawa Saba, anajikuta akianza kupokea upinzani mkubwa kutoka kwa vijana wengine wauni ambao nao wanahitaji utawala wa eneo la Mabibo.
Anafikiria zaidi, jibu ambalo anaamua ni kukusanya vijana wengi zaidi kuwafundisha wizi, kisha kuwa na utawala ambao watu wengine watauogopa. Anaamini atakuwa na nguvu sababu makosa mengi watafanya wengine kwa kupitia yeye.
Hii ndiyo tamthilia mpya ambayo kuna kila aina ya visa na mikasa hasa kwa maisha harisi ya Mabibi. Tukutane ndani ya MABIBO MABWAWA 7 chini ya kampuni yako mpya ya filamu ya GOMESA ENTERTAIMENT.

No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi