BAADA ya kuchaguliwa Ubunge, hii ndio kauli ya kwanza ya mwaasisi wa Muziki wa kizazi kipya wa Bongo Fleva, na sasa mbunge mtarajiwa wa jimbo la Mikumi huko Morogoro.
Naanza Kwa kumshukuru sana Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehma kwa kuniwezesha
kufika mahali hapa nikiwa mzima na mwenye afya njema na kunipigania katika kila
vikwazo na changamoto mbalimbali nilizopitia.
Pili napenda kuwashukuru sana
wananchi wote wa jimbo la langu MIKUMI kwa kuniamini, Kunichagua na kunipa
Heshima hii ya kipekee na dhamana hii ya kuwatumikia, Nawaahidi nitashirikiana
nanyi kwa unyenyekevu mkubwa, kwa nguvu zangu zote na uwezo wangu wote bila
kujali itikadi za vyama vyetu, Maana Lengo letu kuu ni kuleta mabadiliko na
maendeleo ili tuweze kuijenga MIKUMI tunayoitaka,
Mwisho kabisa napenda
kuwashukuru sana Ndugu, Jamaa na Marafiki zangu wote kwa kuonyesha Upendo na
ushirikiano wa nguvu kwa namna moja ama nyingine mpaka kunifikisha hapa nilipo
sasa... MIKUMI MPYA KWA MAENDELEO YA WATU WOTE! Mungu awabariki sana, ASANTENI
SANA!!!! (MBUNGE WA MIKUMI) Mp JOSEPH HAULE...

No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi