Tatizo la
wasanii wa muziki wa kizazi kipya, hususani wale wa muziki wa Hip Hop,
kulalamika kuibiwa kazi zao ingawa kudai kwamba kazi zao ni nzuri na kumewapelekea wasanii wa makundi mawili
kuungana ili kufanya kazi zao pamoja.
Makundi hayo
kutoka mkoani Arusha, moja likitambulika kama Nako 2 Nako lenye makazi yako
Ololo au Kololeni, ambapo mwanzo lilikuwa likiundwa na Ibra De Hustler , Isic Maputo
‘Lord eyes’, George Sextus ‘G Nako’ na wengine.
Wakaungana
na kundi la Liver Camp, ambalo lenye makazi yake Daraja mbili likiundwa na
ndugu wawili Dickson Simon’Niki wa pili’, na John Simon ‘Joh Makini’.
Kuungana kwa
makundi hayo mawili, ndipo likazuka kundi jipya ambalo kwa sasa ndilo kundi
ambalo linafanya vizuri kwenye tasnia ya muziki wa kizazi kitika mtindo wa Hip
Hop.
Akizungumza
mmoja wa kundi hilo George Sextus ‘G Nako’, amesema kwa sasa kundi hilo
linawasanii watano, akiwa Lord Eyes, Nikki wa Pili, Joh Makini na Bonta.
Anasema
kuungana kwa makundi hayo na kutokea kwa kundi hilo, ni kukusanya nguvu ili kuweza kukabiliana na
matatizo ambalo yamekuwa yakiwakuta wanamuziki wa Hip Hop.
Akizungumzia
kuhusu matamasha, alisema kwa sasa tayari wameshaanzisha kampuni ambalo
imesajiliwa kwa jina la Weusi, huku wakiandaa matamasha yao wenyewe.
“Sasa hivi
tumekuwa tukiandaa matamasha yetu, na kila kitu tunafanya wenyewe” anasema.
Anasema
katika kuandaa matamasha huwa wanakutana na changamoto nyingi, kuotokana na
makampuni mengi yamekuwa yanasua sua juu ya kuwaunga mkono.
Hivyo
kutokana na makampuni hayo kutokuwa na ushirikiano wa moja kwa moja, wamejikuta
wakiandaa kwa fedha kutoka mfukoni mwao.
G Nako
anasema changamoto nyingi katika kuandaa tamasha, huwa wanakumbwa na wasi wasi
sana, kama fedha zao zitarudi au laa
hasa kutokana na kila kitu kutoka kwenye mikono yao.
“Ujue
kuandaa kitu kwa fedha zako kuna hitaji moyo, kwakuwa unakuwa unawekeza fedha
nyingi tatizo lipo karika kurejea kwa fedha hizo” anasema.
Kuhusiana na
matatizo la wasanii wengi wa Hip Hop kulalamika nyimbo kutopewa kipaumbile kama
muziki mwingine.
G Nako
anasema umeshapita muda wa kulalamika, ilimradi kila msanii ajue njia gani
azitumie ili kazi yake ifike kirahisi kwenye vyombo vay habari.
“Muda wa
kulalamika umeisha, kila mtu anajua ni jinsi h=gani ya kufikisha kazi zake
kwenye vyombo vya habari na kupigwa kwa kazi zao” anasema.
Anasema wao
kazi zao zimekuwa zikipigwa bila ya wasi wasi kwakuwa wamekuwa wanafanya kazi
nzuri.
Pia msanii
huyo amesema katika kampuni hiyo, ya weusi kwa sasa wanatengeneza T-shit ambazo
wanasambaza kupitia maduka makubwa ya nguo, na zingine wanasambaza kwenye vyuo
ambapo wanamashabiki wengi.
“Huwa
tunawauzia jumla watu wenye maduka makubwa na wao wanauza kwa bei wanazotaka
wao, popote pale” anasema.
Zaidi ya
T-shit anasema kwa sasa kampuni hiyo, imeshaanza kujipanga kutengeneza, kofia,
soksi, boksa na nguo zingine kwaajili ya kuzisambaza zaidi kila sehemu.
Anasema
lengo lao kwa sasa kampuni hiyo kuweza kuitanua na kufanya vitu vinyi, na sio
kutegemea muziki kwa kila kitu, kwakuwa mziki wenyewe unaenda na kubadilika.
Kuhususiana
na watu ambao wamekuwa wakidhamini kutengeneza kazi zao, kama muziki na video
ambazo kwa sasa ‘zimekuwa na ghalamaku bwa.
G nako
alisema kupitia kampuni yao, wamekuwa wakisaidiana sana kuandika nyimbo, na huwa wanapeana
nafasi ya kutoa wimbo jambo ambalo linawafanya waendelee kubaki kileleni kwa
muda mrefu.
Hivyo
amesema hata video zao, pia huwa wanashirikiana kufanya moja baada ya nyingine
na kukamilisha kwa muda muafaka.
“Huwa
tunasaidiana na washikaji katika kukamilisha video zetu, lakini kwa kiasi
kikubwa sana wausika tunakuwa wenyewe” anasema.
Anasema kwa
sasa kampuni yao inaandaa video nne,
mbili wanafanyia Arusha na mtayarishaji Nisha, ambapo kwa sasa
wapokwenye hatua za mwisho.
Anasem baada
ya hapo wanatarajia kufanya video ya wimbo
Bei ya mkaa, ambapo watafanya na Adam Juma wa Next level.
“Video ya
mbili zingine ikiwemo Nikumbatie, ingawa bado hatujajua tutafanya na nani, ila
nategemea mtayarishaji atatoka nje” alisistiza G Nano.
G nako
anasema kupitia kampuni yao ya Weusi anasema, wamekuwa wakijiepusha sana na
mabifu, au ugfonvi ambao kwao hauna tija.
Ugonvi
anasema ndio umekuwa ukirudisha nyuma muziki wao, na hata wale wanaousikiliza
wanaona kama wote wahuni na ndiyo maana hata mara kwanza walikuwa na vikwanzo
vyingi kwa wazazi.
Anasema kwa
sasa kampuni yao itaendelea kusimamia matamashao yao, na kuangalia vyanzo
vingine vya mapato ikiwemo milio ya simu maarufu kama Ring tone.
Anasema
kuhusu mgogoro wa ringtone, unakuja kutokana na wasanii wanafanya kazi kubwa
lakini wanunuzi wa ring tone wanachukua fedha nyingi sana.
“Biashara ya
Ringtone inatoka sana watu wananunua, lakini tukija kwenye kugawanya fedha
zilizopatikana wao wanachukua mapato mengi, na ukiwauliza watakuambia kuna
vijikato vidogo vido kama kodi na vingine” aliendelea kuelezea G Nako.
Katika suala
zima la kuuza ringtone, anasema mwaka huu watahakikisha wanalikalia chini na
kujaribu kujadili kama wataweza kukukbaliana, kwakuwa makato mengine anasema
kwao hayana maana.
G nako
anasema katika mwezi huu anatarajia mwezi huu, wanatarajia kufanya kazi nyingi
kwa kila msanii, lakini ikianza yake akimshirikisha Lord Eyes na mzee Kiki.
Mwisho
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi