Wednesday, January 8, 2014

Isha Mashauzi, kutoa albamu mbili kwa mpigo




MKURUGENZI wa bendi ya Mashauzi Classic, Isha Ramadhani ‘Isha Mashauzi’, amesema anatarajia kuzindua albamu mbili kwa pamoja kama zawadi kwa mashabiki zake.

Isha alisema kwa mwaka huu amejipanga kufanya kazi nyingi zaidi,  ndiyo maana ameamua kutoa albamu hizo mbili, Wasafi wa Mavazi wachafu wa Nafsi na Asiyekujua Akuthamini.

Alisema wasubiri mashabiki wake kwani kuna vitu vipya ndani ya albamu hiyo, ambayo kamwe hakuvifanya mwaka jana.

“Mashabiki wasubiri kazi nzuri zinakuja, nitajitahidi kufanya kazi ambazo wamekuwa wakizitaka wao” alisema.

No comments:

Post a Comment

https://www.facebook.com/gomesamohamedi