Wasanii wa
kundi la Bongo Movies majuzi wamechagua viongozi wapya, ambao watakaoongoza kwa
muda wa mwaka mmoja, huku wakiwa na malengo ya kuifanya taasisi hiyo kuweza
kutanuka zaidi.
Kiongozi ambaye
kwa sasa amechukua nafasi ya mwenyekiti Steve Mangele ‘Steve Nyerere’ akisaidiwa na Muhusin Awadhi ‘Dr
Cheni’ kama mwenyekiti msaidizi, katibu
au mtendaji mkuu nafasi iliyochukuliwa na William mtitu, makamu wa katibu
Devota Mbaga.
Nafasi ya
Hazina imeshikwa na Issa Mussa ‘Cloud 112’ huku akisaidiwa na Sabrina Lupia
‘Cath Lupia’ nafasi ambayo mara kwa mara imekuwa na mgogoro mkubwa.
Viongozi
walioingia katika awamu hii, wengi walikuwa hawana wapinzani kwakuwa waliokuwa
wapinzani walijitoa akiwemo, Hisani Muya, na hivyo walijikuta wakisimama mmoja
mmoja, jambo ambalo wakapitisha mtu atakayekatailiwa kwa nusu ya kula basi atakuwa ameshindwa uchaguzi huo.
Makubaliano
hayo yalipelekea wagombea hao kujikuta katika wakati mgumu, wapiga kura walikuwa 47, na kura zilikwenda
Cath Lupia, alipata kura 41, 3 ziliharibika na 3, zilimkataa, Cloud 112 alipata
46 na mmoja iliharibika, William Mtitu kura 33, akichuana na Wastara Juma
aliyepata kura 13 na mmoja iliharibika.
Dokta Cheni
alipata kura 41 tano zilimkataa na mmoja iliharibika, wakati Steve Nyerere
alipata kura 40 tatu zilimkataa na nne ziliharibika.
Hata hivyo
Sela mbalimbali zilitangazwa katika kuwania vyeo hivyo, nahata wagombea
walichemshana kwa kuongea wazi kwamba hawezi kufanya kazi na mtu fulani
kulingana na sera zake, ingawa sera kwa upande mwingine watu walizipenda.
Miongoni mwa
sera ambayo ilipendwa na wengi, ikawa kama sehemu ya kushangilia, ni ile ya
William Mtitu, mtu ambaye anasifika kwa umakini na ukali wa hali ya juu
alipotangaza.
Watu
walipomuuliza kuhusiana na hasira zake, na jinsi alivyoweza kumpeleka msanii
mwenzake polisi jambo ambalo alilijibu kwa kujiamini na kusema.
“Kama
mnataka kunipa kura nipeni, lakini kama mnahisi viongozi wataiba mali ya Bongo
Movie, huku mimi naona nikiwa kama mtendaji mkuu basi lazima niwapeleke polisi.
Suala la suruhisho tutasuruhishana lakini suala la wizi lazima wafike polisi,”
alisema Mtitu.
Kutokana na
sera hiyo, alijikuta akipata ufuasi wa watu wengi ambao wengi wao waliokuwa
wakilalamika, wapi fedha zilipoenda zile za mara kwanza.
Sera
iliyokuwa ikitikisa na lilikuwa tumaini kubwa kwa wasanii wa Bongo Movie, ni
ile ya Steve Nyerere ya kuanza kugomea, fedha chache wanalipwa watengenezaji
filamu.
Hata alisema
lazima aitishe mkutano mkubwa wa watengenezaji filamu nchini, na wasambazaji
ili kujua ni jinsi gani wasanii wanavyoweza kurekebishiwa haki zao na hata
kutouza haki miliki.
“Mimi
nitakuwa mtu wa kwanza kugoma na mimi nitakuwa mtu wa kwanza kufokea, pale
msanii atakapoonewa kwa hali yoyote kwa kuuza haki zake” Steve Nyerere
alisisitiza.
Pia alisema
miongoni mwa sera zake ni kuita Bodi ya wazamini, ambayo atakusanya matajiri
mbalimbali ambao wataweza kuja kudhamini Bongo Movies, na hata kufanya mechi au
michezo ya ghalama kwaajili ya kuchaza mfuko wao.
Hata hivyo
kikubwa kilichowapa tumaini kwa wasanii wa filamu juu ya kauli ya mwenyekiti
huyo mpya, pale alipokuja kuchukua fomu ya uongozi akisindikizwa na msafara wa
matajili wanaouza magari mjini na watu maarufu.
Mikakati
mbalimbali ambayo kwa sasa ndiyo tumaini la wasanii wengi wa Bongo Movie, ilipo
ni juu ya mipango mipya kwa wasanii wote.
Miongoni ya
mipango hiyo, ni kujenga ofisi ya Bongo Movie ambayo itakuwa maalum kwaajili ya
wasanii kukutaniana hapo na kuendesha mikutano yao.
“Mimi na
nyinyi tutashirikiana kuhakikisha tunapata eneo zuri la Ofisi, ambapo tutakuwa
pia tukifanya mikutano yetu” alisema Steva.
Pia
walipanga kufungua akauti ya benki ya Bongo Movie, ambayo haikufunguliwa tangu
ilipoanza kwa taasisi hiyo.
Wanasema
akauti ya benki itakuwa ikifunguliwa na watu , ambao ndio watakuwa wakisaini
juu ya utokaji wa fedha, akiwa mweka hazina msaidizi, katibu na mwenyekiti
wake.
Mikakati
mingine waliyoipanga ni kuhakikisha safari za mikoani au za kimichezo,
anakwenda mtu yoyote ambaye mwanachama na sio kwenda mtu kulingana na umaarufu
wake, wakati kwenye vikao haudhulii.
Hata hivyo
wapo pia waliolalamika kutochezeshwa katika filamu jambo ambalo nalo walisema
lazima kila anayetengeneza filamu kutoka katika chama hicho achukue wasanii
kuanzia watutu na kuendelea kutoka humo humo.
Miongoni mwa
changamoto ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na wasaniii wengi, hasa kutoka katika
uongozi uliopita wa Visent Kigosi, na kuamini huenda ukaendelea hadi katika
uongozi huu mpya.
Changamoto
hizo ni wasanii kuchukuana katika safari za mikoani, wakiwa wawili waili yaani
wenye uhusiano jambo ambalo, wengi hawakulitaka kulijibu kama lilivyotakiwa na
kulikwepa.
Swali
lingine ambalo lilikuwa na mjadala mkubwa ni kuhusiana na kuliwa kwa fedha za
michezo ambazo zilipita, kama za Mpira wa Miguu, na Net ball, ambazo hadi leo
wanadai hawajui zilipo.
Changamoto
kubwa nyingine ambayo uongozi wanakumbana nayo, ni kuhusu mpasuko wa wasaniii
wakubwa kuwa na makundi, ambayo mara nyingi yamekuwa yakisababisha kudumaa na
kutaka kufa kwa taasisi hiyo.
Hata hivyo
mwisho wa siku uongozi mpya umesema yaliyopita si ndwele, tugange yajayo baada ya kila mmoja kukiri kwamba alitenda
makosa kwenye uongozi wake.
“Mimi
nawashauri uongozi ujao, wasifanye kama yale tuliofanya katika uongozi wetu.
Watu tulikuwa tukijadiliana na wengine walikuwa wakienda kuongea nje na kusema
juu ya kile tulichopanga. Ni mara nyingi ubaya wote ulirudi kwangu” alisema
Vicent Kigosi ‘Ray’ Mwenyekiti aliyemaliza uongozi wake.
Bongo Movie
Unit ilianzishwa mwaka 2011, ikiwa chini ya watu watatu akiwa Jimmy
Mafufu, Captu Radon a Ben Kinyaiya.
Baada ya
hapo waliaamua kuifikisha kwa watu wengine, ambapo ikaungana na kuwa ya watu
tisa, chini ya uongozi wa Athuman Mbilinyi, akiwa mwenyekiti, na makamu wake
Jacob Stephan, katibu Ben Kinyaiya makamu Captu Rado, mtunza hazina Single
Mtambilike, msaidizi wake Vicenti Kigosi.
Mwaka 2012
Uongozi ukaja ukabadilika baada ya uchaguzi na Mwenyekiti akawa Jacob Stephan
‘Jb’, makamu Athuman Mbilinyi, katibu Cloud 112, makamu Jackline Wolper, mweka
hazina Single Mtambalike na msaidizi wake Vicent Kigosi.
Mwaka 2013 viongozi Vincent
Kigosi aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti
Mkuu, Irene Uwoya -Makamu wa Mwenyekiti , Chiki Mchoma
Katibu Mkuu, Single Mtambalike aka Richie Richie alichaguliwa kuwa Mtunza Fedha
Mkuu na Makamu wake kuwa Jackline Wolper.
Mwisho
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi